Je umegundua vitufe vipya vya Facebook?

Image caption Vitufe vipya vya Facebook

Je umegundua vitufe vipya vya Facebook ?

Kuanzia leo mtandao wa kijamii wa Facebook umezindua vitufe (emojis) 5 vipya ilikufanikisha watumiaji wa mtandao huu kujieleza kwa kutoa maoni yao kwa usahihi zaidi ima wamefurahia jambo ama hata wamelikataa kwa kubofya picha inayoambatanisha na maoni yao.

Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Facebook bwana Mark Zuckerberg amesema kuwa watumiaji bilioni 1.5 wa mtandao huo wataanza a kutumia vitufe hivyo vipya leo(jumatano).

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kwa zaidi ya miaka 7 saba watumizi wamekuwa wakituuliza tuwape njia zaidi ya kujieleza kwenye Faceboo alisema bwana Mark Zuckerberg

Vitufe hivyo vipya vina picha ya "wow(Furahia)", "penda", "haha(Cheka)", " huzuni" na"yakasirisha".

Kitufe cha ''Like'' ambacho ndicho kilikuwa kibwagizo cha Facebook katika kipindi cha miaka 7 kimesalia hapo kama nembo ya kuwasaidia watumizi kujieleza zaidi katika mtandao wa Facebook alisema bwana Zuckerberg kupitia taarifa aliyochapisha kwenye mtandao wake wa Facebook.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kuanzia leo mtandao wa kijamii wa Facebook umezindua vitufe (emojis) 5 vipya ilikufanikisha watumiaji wa mtandao huu kujieleza

''Bila shaka ninafahamu kuwa sio habari zote unazozipata kupitia kwenye mtandao wa Facebook ni za kufurahisha (like) ndio sababu tumekupa hizi zingine kukuwezesha kujieleza kwa njia sahihi zaidi katika Faceboook.

''Kwa mtazamo wangu kitufe cha kupenda ndicho kilichotumika sana haswa katika kipindi cha majaribio'' alisema mkurugenzi huyo wa facebook.

Nasi hapa BBCSwahili.com tunakuuliza je umezipokeaje vitufe hivyo vipya ?

Tuachie maoni yako kwenye mtandao wetu wa Facebook tafuta BBCSwahili.