Kimbunga Fiji:Waliofariki wafika 42

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Madhara ya kimbunga cha fiji

Idadi ya watu waliofariki kufikia sasa katika janga la kimbunga kilichopiga kisiwa cha Fiji Jumamosi iliyopita imepanda na kufikia 42.

Maafisa nchini humo wanahofu kuwa huenda idadi hiyo ikapanda zaidi, kwani data za watu waliofariki zinatoka maeneo ya ndani zaidi vijijini.

Nyaya ya nguvu za umeme iliyokuwa imekatizwa sasa inaunganishwa huku vyumba vya kuhifadhia maiti vikiwa bado havina umeme.

Kwa sababu hiyo, serikali sasa imezishauri familia zilizopoteza wapendwa wao, kuwazika au kuzichoma maiti haraka iwezekanavyo, kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya kuhifadhi maiti.