Rubani akanusha kumshambulia polisi Kenya

Video Haki miliki ya picha Citizen TV Kenya RMS
Image caption Video iliyodaiwa kuonyesha yaliyotokea ilisambaa sana mtandaoni

Rubani aliyetuhumiwa kumdhalilisha afisa wa polisi wa kike eneo la Nyandarua, nchini Kenya amefikishwa kortini na kukanusha mashtaka.

Bw Alistair Alistair Llewelyn ameshtakiwa kwa makosa mawili, moja la kumshambulia afisa wa polisi na jingine la kuvuruga amani na kutoa matusi.

Hakimu katika mahakama ya mji wa Engineer, Nyandarua ameagiza awekwe rumande hadi Jumatatu wiki ijayo kuwawezesha maafisa wa uchunguzi kupata habari zaidi ikiwemo kuthibitisha uraia wake.

Bw Alistair Llewelyn alijisalimisha kwa polisi eneo la Kilimani, Nairobi siku ya Jumatatu na akasafirishwa hadi mji wa Engineer, katikati mwa Kenya kujibu mashtaka kuhusiana na tukio lililotokea Jumapili katika eneo la Ndunyu Njeru kilomita chache kutoka mji wa Engineer wakati wa mkutano wa Naibu Rais William Ruto.

Kisa hicho kilinaswa kwenye video ambayo ilisambaa sana mtandaoni.