Afrika Kusini kuondoa jeshi lake Darfur

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Taifa la Afrika Kusini litaondoa jeshi lake la kulinda amani katika eneo la Darfur nchini Sudan kutoka mwezi April 1, afisi ya rais Jacob Zuma imesema katika taarifa yake, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Jeshi hilo limekuwa Darfur tangu mwaka 2008 kama mojawapo ya vikosi vilivyoa nzishwa na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika ili kusitisha vurugu katika nchi hiyo.

Mwaka Jana, serikali ya Afrika Kusini ilikaidi amri ya mahakama ya kukataa kumkamata Rais wa Sudan Omar al-Bashir,ambaye anahitajika na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kwa shtaka la mauaji ya kimbari.

Bwana Bashir amekana mashtaka hayo.