Donald Trump ashinda Nevada

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda katika jimbo la Nevada nchini Marekani, na hivyobasi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.

Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu ,kufuatia ushindi wake katika jimbo la New Hampshire na Carolina kusini.

Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.

Maafisa wa chama hicho wamesema wamekuwa wakichunguza ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.

Baadhi ya watu waliojitolea pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za bwana Trump,lakini maafisa wamesema kuwa hatua hiyo sio kinyume na sheria.