AU kukamilisha mazungumzo ya amani Burundi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Jacob Zuma

Viongozi wa mataifa matano ya Afrika wanaokwamua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi wanakamilisha mazungumzo yao katika mji mkuu wa taifa hilo Bujumbura.

Usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa,viongozi hao walikutana na wanasiasa,wanaharakati na makundi ya kidini.

Image caption Jacob Zuma na Pierre Nkurunziza

Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge amesema kuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliwaambia wanasiasa hao kwamba lengo lao kuu ni kuunga mkono juhudi za kuleta amani nchini humo.

Bwana Zuma na rais Pierre Nkurunziza wanatarajiwa kutoa taarifa mwishoni mwa ziara hiyo.