Unene kupita kiasi hudhoofisha uwezo wa kukumbuka

mwanamke mnene na mwembamba Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watu wenye unene wa kupita kiasi hawakumbuki sawa na wenzao walio wembamba

Watu wanene kupita kiasi wana kumbu kumbu mbaya zaidi kuliko wenzao wembamba zaidi, utafiti mdogo umeonyesha. Uchunguzi uliofanywa kwa watu 50 ulionyesha kwamba kuwa mmene kupita kiasi kulikua na uhusiano na '' kumbu kumbu ya msururu wa matukio " ama uwezo wa kukumbuka mambo yaliyopita.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Unene unaosababishwa na chakula unaweza kuchochea mtu kula kupita kiasi

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Experimantal Psychology, unadai kwamba kumbu kumbu ndogo zaidi inayosababishwa na milo ya hivi karibuni inaweza kusababisha ulaji wa kupita kiasi.

Hata hivyo, masuala mengine yanayochangia mtu kuwa na kumbu kumbu ndogo kama vile uelewa wa mambo kwa ujumla hayakuangaziwa na utafiti huu.

Haki miliki ya picha Don Mammoser Alamy
Image caption Vipimo vilivyochukuliwa kwenye panya vilionyesha kua walionenepa zaidi hawakua na kumbukumbu nzuri

Vipimo walivyofanyiwa panya awali vilionyesha kwamba waliokua na unene zaidi walishindwa kufanya vizuri katika vipimo vya kumbu kumbu, lakini ushahidi kwa binadamu umekua na matokeo tofauti tofauti.

Utafiti wa hivi karibuni uliangazia zaidi kumbu kumbu za matukio katika mfulurizo -kama mkanda wa video katika ubongo wako - ambao hukumbuka harufu ya kikombe cha kahawa ama hisia za kushika mkono wa mtu mwingine.