Wanajeshi wabakaji wafungwa jela Guatemala

Haki miliki ya picha AP
Image caption Guatemala

Mahakama kuu nchini Guatemala imewahukumua wanajeshi wawili wa zamani kifungo cha mamia ya miaka gerezani kwa kuwabaka na kuwafanya watumwa wanawake wa asili wakati wa mzozo wa miaka ya 80 nchini humo.

Kamanda wa zamani wa kambi ya Sepur Zarco na mkuu wa majeshi Heriberto Valdez Asij waliwalazimisha wanawake hao kufanya kazi kwa zamu wakipika na kufanya usafi wakati ambapo pia walibakwa na wanajeshi katika kambi hiyo.

Wawili hao walipatikana na hatia ya kuwaua waume wa wanawake hao baada ya kushtumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa mrengo wa kushoto.