Usitishwaji wa vita waanza kutekelezwa Syria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Syria

Kumekuwa na usitishwaji wa mapigano usiku kucha nchini Syria baada ya makubaliano ya kusitisha dhuluma kuanza kutekelezwa.

Maeneo ya mbele ya vita katika mji ulio kaskazini wa Allepo yaliripotiwa kutulia mapema asubuhi huku nao mji wa Damascus na vitangoji vyake vikiripotiwa kutulia.

Lakini wanaharakati wanasema kuwa na makabiliano ya hapa na pale kati ya serikali na waasi katika mkoa wa pwani wa Latakia

Vyombo vya habari vya serikali vilisema kuwa bomu la kutegwa ndani ya gari liliwaua watu wawili katika mkoa wa Hama

Usitishwaji huo mkubwa tangu miaka mitano iliyopita haushirikishi wanamgambo wa Islamic State na kundi la Nusra Front lililo na uhusiano na Al Qaeda.