Shambulio la angani lawauwa watu 30 Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shambulio Yemen

Takriban watu 30 wameuawa katika shambulio la angani ndani ya soko moja karibu na mji mkuu wa Yemen Sanaa,kulingana na mashahidi.

Wakaazi walinukuliwa na shirika la habari la Reuters wakisema kuwa takriban watu 30 wamejeruhiwa wengi wakiwa raia .

Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulio hilo.

Takriban watu 6000 wameuawa tangu muungano wa kijeshi unaoongozwa na taifa la Saudia kuanza kuwashambulia waasi mwezi Machi.

Mashambulio hayo yanalenga kuirejesha mamlakani serikali na kuwafurusha waasi wa Houthi wanaomuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Ali Abdullah Saleh.