Mji wa India wapiga marufuku filamu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa kaskazini mwa India, Aligarh, umepiga marufuku filamu mpya ya wapenzi wa jinsia moja

Mji wa kaskazini mwa India, Aligarh, umepiga marufuku filamu mpya yenye jina la mji huo, kuoneshwa huko, kwa sababu inahusu mapenzi ya jinsia moja.

Meya wa mji huo Shakuntala Bharti, alisema jina la filamu linafaa kubadilishwa, kwa sababu linahusisha mji huo na mapenzi ya jinsia moja, na hivo, kama alivosema, inautusi mji.

Chama cha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Waislamu mjini huimo, wamekariri maoni yake.

Filamu hiyo inahusu maisha ya profesa wa chuo kikuu, ambaye alisimamishwa kazi, kwa sababu alifanya mapenzi ya jinsia moja, na baadaye alijiuwa.

Aliyetengeneza filamu hiyo, Hansal Mehta, amesema malalamiko yanayofanywa ni "chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja".