Wafuasi wa Rouhani washinda viti vyote Tehran

Image caption Wandani wa rais anayependelea mabadiliko nchini Iran, Hassan Rouhani, wameshinda viti vyote 30 mjini Tehran

Wandani wa rais anayependelea mabadiliko nchini Iran, Hassan Rouhani, wameshinda viti vyote 30 mjini Tehran katika uchaguzi wa wajumbe.

Uchaguzi huu ndio uliokuwa wa kwanza tangu vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran kuondolewa kufuatia nchi hiyo kutia sahihi mapatano ya kuthibiti nguvu za nukilia na mataifa ya dunia.

Baada ya kuhesabiwa kwa kura asilimia 90, wafuasi wa rais Rouhani waliokuwa wamepigiwa upatu kuibuka washindi al maaruf ''List of Hope'', wanatarajia kushinda viti vyote 30 katika jiji kuu la Tehran.

Wafuasi wa Rouhani wanaendelea pia kufanya vizuri katika maeneo yanayozingira mji mkuu.

Bwana Rouhani amesema kuwa uchaguzi huo umeiongezea nguvu serikali yake ambayo imepongezwa kwa kutafuta mwafaka ulioiruhusu Iran kuanza kuuza mafuta yake katika soko la dunia.

Kiongozi mwenye msimamo mkali na asiyependelea mabadiliko Gholamali Haddad-Adel ameshikilia nafasi ya 31.

Hata hivyo hali huenda ikawa mchanganyiko katika miji mingine midogo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tayari kura zimepigiwa baraza la wataalamu 88, linalowashirikisha wahubiri wanaomchangua kiongozi mkuu wa kidini nchini humo.

Tayari kura zimepigiwa baraza la wataalamu 88, linalowashirikisha wahubiri wanaomchangua kiongozi mkuu wa kidini nchini humo.

Baraza hilo ndilo litakalomchagua kiongozi atakayerithi kiongozi wa kidini Ayatollah Khamenei, ambaye anaugua kutokana na umri wake mkubwa.

Khamenei anaumri wa miaka 76.

Ushindi katika mji mkuu wa Tehran unamaana zaidi ya moja kwani wabunge wa mji huo huwa na ushawishi mkubwa wa jinsi mambo yanavyoendeshwa kule majimboni.

Haki miliki ya picha BBc
Image caption Wafuasi wa Rouhani wanaendelea pia kufanya vizuri katika maeneo yanayozingira mji mkuu.

Aliyekuwa rais wa nchi hiyo bwana Akbar Hashemi Rafsanjani,mshirika wa rais Rouhani ni miongoni mwa wale waliopata ushindi katika uchaguzi huo.

Kiongozi wa wenye msimamo mkali na mpinzani sugu wa rais Rouhani bwana Ayatollah Taghi Mesbah Yazdi, alikuwa hana hakika ya ushindi wa moja kwa moja.