Serikali mseto ya Ireland yavunjika

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri Mkuu wa Ireland, Enda Kenny

Waziri Mkuu wa Ireland, Enda Kenny, amekiri kuwa serikali yake ya mseto imeshindwa katika Uchaguzi Mkuu wa Ijumaa.

Bwana Kenny alisema ni dhahiri kutokana na matokeo ya hivi sasa kuwa muungano kati ya chama chake cha Fine Gael na kile cha Labour hauwezi kuidhinishwa tena.

Lakini licha ya kushindwa vibaya, chama chake cha Fine Gale kinatarajiwa kuwa chama kikubwa zaidi nchini.

Kuna uvumi kuwa huenda kikaungana na chama cha Fiana Fail, kinachotarajiwa kushikilia nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu.

Image caption Kuna uvumi kuwa huenda kikaungana na chama cha Fiana Fail

Waandishi wa habari kutoka eneo hilo wanasema walionufaika zaidi katika Uchaguzi huo ni vyama vidogo vidogo na vile vya kujitegemea.

Vyama hivyo vimenufaika kutokana na juhudi za waziri mkuu Kenny kubana matumizi ya umma.