Bwana harusi mlevi alazimu ndege kutua

Haki miliki ya picha
Image caption Bwana harusi mlevi alazimu ndege kutua

Wanaume 6 waliokuwa katika karamu ya kumuaga bwana harusi walilazimika kutafuta usafiri mbadala baada ya wahudumu wa ndege ya Ryanair kuwatimua katikati ya safari.

Wanaume hao 6 raia wa Uingereza walikuwa wakielekea Bratislava lakini polisi wa Ujerumani walishukishwa kwa lazma mjini Berlin Ujerumani baada ya wahudumu wa ndege walimokuwa kushindwa kustahimili mihemko yao wakiwa walevi.

Wanaume hao wenye umri kati ya miaka 25-28, walikuwa baadhi ya ujumbe wa watu 12 waliokuwa wakielekea katika mji mkuu wa Slovakia kutoka London ijumaa.

Walioshuhudia wanasema kuwa wahudumu walishindwa kuwadhibiti baada ya kubugia mvinyo wakiwa angani.

Walilazimika kutua Berlin Ujerumani na kuwatumia polisi kuwaburuta iliabiria wengine waliokuwa katika ndege hiyo waendelee na safari yao.

Cha ajabu ni kuwa Bwana harusi alikuwa mmoja kati ya 6 waliotiwa mbaroni kwa utovu wa nidhamu na kuhatarisha maisha ya abiria wengine.

Vyanzo vya polisi vinasema kuwa 6 wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa harusi, waliendelea na safari yao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa Ujerumani wanasema walishikwa kwa sababu walikaidi amri ya kuketi chini

Polisi wa Ujerumani wanasema walishikwa kwa sababu walikaidi amri ya kuketi chini na kuwa mmoja wao alikuwa keshavua nguo.

Mambo yalienda segemnege wahudumu wa ndege walipokataa kuwapa mvinyo zaidi wakidai walikuwa wameshalewa chopi.

Polisi katika uwanja wa ndege wajerumani Schoenefeld Berlin waliwafungulia mashtaka ambayo watalazimika kulipa faini ya hadi pauni elfu £20,000.