Ghasia Ufaransa ikivunja kambi ya wahamiaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ghasia Ufaransa ikivunja kambi ya wahamiaji

Kumekuwa na makabiliano makali kati ya wahamiaji na polisi wakati kikosi cha wafanyikazi wa ufaransa walipokuwa katika shughuli ya kubomoa maakazi ya muda ya wahamiaji katika mji wa Calais huko Ufaransa.

Magari aina ya bulldozer yametumiwa katika bomoabomoa hiyo ya eneo hilo la wakimbizi liliobandikwa jina la the 'Jungle'.

Imebidi polisi wa kuzuia ghasia kufytua mabomu ya kutoa machozi kukabiliana na vijana wahamiaji waliokuwa wakiwarushia mawe.

Wakimbizi waliokuwa wakiishi katika sehemu hiyo waliamuriswa kuondoka baada ya utawala wa mji wa Calais kupata kibali cha mahakama cha kubomoa makaazi hayo yasiyo rasmi.

Haki miliki ya picha
Image caption Polisi wanasema wanawataka wahamie sehemu nyengineyo.

Polisi wanasema wanawataka wahamie sehemu nyengineyo.

Hata hivyo wakimbizi hao wanataka kubaki walipo kwa lengo la kudandia misafara na kuelekea Uingereza .

Wengi wao wametoroka vita makwao hasa Syria na Afghanistan.