Serikali ya Marekani yasutwa kuhusu Apple

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kampuni ya Apple

Jaji mmoja mjini New York ametoa uamuzi kuwa serikali ya Marekani haiwezi kuilazimisha kampuni ya Teknolojia ya Apple, kupatia shirika la ujasusi la Marekani FBI uwezo wa kufungua simu za iPhone zilizotumiwa katika visa vya mihadarati.

Serikali ilitaka ipewe uwezo wa kufikia taarifa za simu hizo mwezi October ikiwa ni mwezi mmoja kabla jaji wa California kuamuru Apple kusaidia kufungua simu ya iPhone ya raia mmoja aliyeuwaua watu 14 .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kesi ya Apple

Apple imesema FBI inataka mamlaka hatari na hatua ya kuvunja haki za kikatiba .

Kesi hiyo ya California ilizua mjadala wa kitaifa nchini Marekani juu ya uwiano kati ya usalama na haki ya mtu kuwa na mambo yake binafsi .