Uchaguzi mpya wa urais watangazwa Myanmar

Haki miliki ya picha AP
Image caption Aung san Suu Kyi

Maafisa nchini Myanmar wametangaza uchaguzi wa rais mpya katika muda wa wiki moja.

Sasa uchaguzi huu utafanyika tarehe 10 mwezi huu ma Machi.

Mwandishi wa BBC nchini Myanmar anasema uamuzi huu ambao ni wa ghafla una maanisha kumalizika kwa majaribio ya kuahirishwa ama kubadilisha katiba kwa ajili ya kumruhusu Aung San Suu Kyi kuwa rais mpya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wabunge wa Myanmar

Chama cha Aung San Suu Kyi cha National League for Democracy kilishinda katika uchaguzi , lakini kulingana na sheria za sasa ambazo zilizobuniwa na utawala wa kijeshi wa Myanmar' haruhusiwi kuwa rais kwa sababu watoto wake wana paspoti za kigeni