MOJA KWA MOJA: Mchujo wa Jumanne Kuu Marekani

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

15:00 Huu ndio mwisho wa habari za moja kwa moja za mchujo wa Jumanne Kuu. Asante kwa kuwa nasi. Kwaheri.

15:00 Ramani ya matokeo katika majimbo ya Jumanne Kuu.

12:00 Seneta Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama cha Republican jimbo la Alaska. Hilo ndilo jimbo lake la tatu kushinda. Majimbo hayo mengine aliyoshinda ni Texas na Oklahoma.

Haki miliki ya picha Getty
11:30 Hali ilivyo kwa wajumbe

Kumbuka, jambo muhimu zaidi katika mchujo wa kuteua wagombea urais watakaopeperusha bendera ya vyama vya Republican na Democratic. Hawa hukusanyika kwenye mkutano mkuu wa vyama na kuidhinisha wagombea.

Kufikia sasa, hivi ndivyo hali ilivyo chama cha Democratic.

  • Hillary Clinton ameshinda 441 kati ya wajumbe 865 walioshindaniwa Jumanne Kuu. Sasa ana jumla ya zaidi ya wajumbe 989.
  • Bernie Sanders anaelekea kushinda wajumbe 262. Sasa ana jumla ya zaidi ya wagombea 349.

Wagombea wa Democratic wanahitaji wajumbe 2,383 kushinda.

Katika chama cha Republican

Kati ya wajumbe 595 waliokuwa wakishindaniwa Jumanne Kuu, hivi ndivyo wagombea walivyobahatika:

  • Trump: angalau wajumbe 186.
  • Cruz: 125
  • Rubio: 62
  • Kasich: 18
  • Carson: 3

Kwa jumla Donald Trump sasa anaongoza akiwa na wajumbe 268, Cruz na 142, Rubio ana 78. Kasich ana 24 na Carson wajumbe wanane.

Wagombea wa Republican wanahitaji wajumbe 1,237 kupata uteuzi.

(Takwimu zimetoka kwa Associated Press).

08:50 Matokeo kufikia sasa:

Donald Trump (Republican): Alabama, Georgia, Massachusetts, Tennessee, Virginia, Arkansas, Vermont

Ted Cruz (Republican): Texas, Oklahoma

• Marco Rubio (Republican): Minnesota

Hillary Clinton (Democrat): Alabama, Georgia, Tennessee, Virginia, Arkansas, Texas, Massachusetts

Bernie Sanders (Democrat): Vermont, Oklahoma, Minnesota, Colorado

08:13 Donald Trump ameshinda jimbo la Vermont, jimbo lake la saba kushinda mchujo wa Republican Jumanne Kuu.

08:07 Bernie Sanders pia ameshinda jimbo la Colorado, jimbo lake la nne chama cha Democratic.

07:47 Bernie Sanders ameshinda jimbo la Minnesota, jimbo lake la tatu kushinda mchujo wa Jumanne Kuu.

07:41 Hillary Clinton ameshinda jimbo la Massachusetts, jimbo lake la saba kushinda mchujo wa Democratic.

Haki miliki ya picha Getty

07:23 Marco Rubio ameshinda jimbo lake la kwanza kabisa katika mchujo wa chama cha Republican. Ameshinda Minnesota.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Marco Rubio amekuwa akijibizana sana na Trump
06:43 Matokeo yalivyo kwa sasa:

Republican:

Alabama: Trump

Georgia: Trump

Massachusetts: Trump

Tennessee: Trump

Texas: Cruz

Oklahoma: Cruz

Virginia: Trump

Arkansas: Trump

Democrat:

Alabama: Clinton

Georgia: Clinton

Tennessee: Clinton

Virginia: Clinton

Vermont: Sanders

Arkansas: Clinton

Texas: Clinton

Oklahoma: Sanders

American Samoa: Clinton

Haki miliki ya picha Reuters.AFP
Image caption Trump ameshinda majimbo saba, Clinton ameshinda majimbo saba na eneo la American Samoa

Matokeo yanayosubiriwa:

Minnesota na Alaska kwa vyama vyote viwili

Massachusetts kwa Democratic

Vermont kwa Republican

06:16 Ted Cruz kwa sasa anahutubu Houston, Texas. Anasema siku ya leo imeingiza kinyang'anyiro cha kutafuta atakayepeperusha bendera ya Republican. Amesema kabla ya leo wagombea wamekuwa wengi lakini mambo yatabadilika. Amesema wanaompinga Trump wakiendelea kugawanyika ndivyo, Trump atakavyoendelea kufana. Anasema kampeni yake, ndiyo pekee inayoweza kumshinda trump.

Haki miliki ya picha Getty

"Tumemshinda mara moja, mara mbili, mara tatu."

06:14 Ben Carson amepangiwa kufanya mkutano wa kampeni Maryland baadaye leo. Bado hajasema iwapo atajitoa kutoka kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa Republican licha ya kutofanya vyema mchujo wa Jumanne Kuu.

06:10 Donald Trump akihutubu Palm Beach, jimbo la Florida amejitetea dhidi ya tuhuma kwamba anawatenganisha watu, na hasa chama chake. Amesema yeye ni mgombea anayetetea "umoja".

06:08 Siku chache zilizopita, Chris Christie, alikuwa mkosoaji mkubwa wa Bw Trump, pamoja na mpango wake wa kujenga ua kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji. Siku chache zilizopita, alijiondoa kutoka kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea.

Sasa, amesimama nyuma ya Trump ambaye anauza sera zake. Mtandaoni, watu wameanzisha kitambulisha mada #FreeChrisChristie (Mkomboeni Chris Christie), wakisema anaonekana kama mateka.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Trump na Chris Christie

06:05 Trump akihutubu amemshambulia Clinton, hasa kutokana na wakati wake alipokuwa waziri wa mashauri ya kigeni. Amegusia mzozo unaoendelea nchini Syria. Trump amesema wengi waliofanya makosa kama ya Clinton tayari wangekuwa wamejutia makosa yao.

06:00 Donald Trump ameshinda majimbo ya Virginia, Alabama, Massachusetts, Georgia na Tennessee.

Haki miliki ya picha Reuters

05:39 Bernie Sanders ameshinda majimbo mawili, Oklahoma na Vermont, katika mchujo wa chama cha Democratic.

Haki miliki ya picha Getty

05:31 Hillary Clinton tayari ameshinda majimbo sita: Alabama, Arkansas, Georgia, Tennessee, Texas na Virginia katika mchujo wa chama cha Democratic.

05:30 Ted Cruz anaelekea kushinda mchujo wa Texas na Oklahoma chama cha Republican.

Haki miliki ya picha Getty
04:35
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hillary Clinton

Hillary Clinton ameshinda majimbo matano katika uteuzi wa mgombea kiti cha Democtratic nchini Marekani.

00:09

Akihutubia mkutano katika jimbo la Minnesota mgombea kiti cha Republican Marco Rubio, amemfananisha Donald Trump na Jesse Ventura, ambaye alichaguliwa kuwa gavana wa jimbo la Minnesota mwaka 1998 baada ya kuhudumu kama mwaanjeshi mwanamaji na pia mwana mieleka.

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Marco Rubio

"Bwana Trump ni mtu maarufu tu kama Ventura," alisema Rubio. Wakati huo huo Bwana Ventura aliliambia gazeti la Daily Beast kuwa atagombea urais ikiwa Bernie Sanders hatapata uteuzi wa chama cha Republican.

NI JUMATANO Afrika Mashariki22:28
Haki miliki ya picha Getty
Image caption Donald Trump

Akiwahutubia wafuasi wake mjini Columbus ,Ohio, mgombea kiti cha Republican Donald Trump amerejela hoja ya kuu ya ''kuifanya Marekani kuwa taifa maarufu na lenye nguvu tena''

Taifa letu limegawanyika sana. Limegawanyika katika misingi ya rangi kati ya weupe na weusi limegawanyika sana''

Nawaomba tuliunganishe tena,lazima tuilete Marekani pamoja''.

19:37 Kando na majimbo 12 ya Marekani, wapiga kura walio ng'ambo wanashiriki mchujo chama cha Democratic. Larry Sanders kakake mgombea wa Democratic Bernie Sanders, amepiga kura yake ya mchujo katika kituo cha Taasisi ya Marekani ya Rothermere, Oxford, UK nchini Uingereza.

Haki miliki ya picha Press Association
Image caption Larry Sanders akipiga kura yake Oxford

19:34 Upigaji kura utamalizika 1900 au 2000 EST (saa sita usiku au 01:00 GMT Jumatano) na matokeo yatatarajiwa kuanzia wakati huo.

Katika jimbo la Alaska, upigaji kura huendelea hadi saa sita usiku EST (05:00 GMT).

Haki miliki ya picha Getty

19:17 Upigaji kura kwa sasa unaendelea. Kuna majimbo 12 yanayochagua wagombea. Baada ya mchujo wa leo, jimbo la Colorado hufanya mkutano mkuu wa chama wa kugawa wajumbe.

19:15 Jumanne Kuu ilianzishwa 1988 kujaribu kutoa taswira kamili ya msimamo wa Wamarekani kuhusu wagombea na uwezo wao. Kwa maelezo muhimu kuhusu siku hii, soma: Mambo 5 muhimu kuhusu Jumanne Kuu

Haki miliki ya picha AFP y Reuters
Image caption Bi Hillary Clinton anaongoza kwa wajumbe chama cha Democratic, na Donald Trump anaongoza kwa wajumbe Republican

19:10 (Saa za Afrika Mashariki) Hujambo! Karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu mchujo wa kuteua wagombea urais wa vyama vya Republican na Democratic katika majimbo 12 nchini Marekani.

Siku hii hufahamika sana kama Jumanne Kuu.