Shutma za rushwa dhidi ya Zuma zafufuliwa

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma

Mahakama nchini Afrika kusini itasikiliza kesi iliyofunguliwa na upinzani kufufua mashtaka 738 dhidi ya Rais Jacob Zuma.

Afisi ya Rais Zuma hata hivyo iimesema itapinga mpango huo, ikisema waendesha mashtaka walipima mizani ya madai hayo kabla ya kuondoa mashtaka hayo mwaka 2009.

Upinzani unaamini kuwa kitendo cha kutupilia mbali mashtaka kilikuwa cha kisiasa, na lengo lilikuwa kufungua milango kwa Rais Zuma kuwa Rais.

Rais Zuma alituhumiwa kupokea hongo ya mabilioni ya dola kwa mradi wa ununuzi wa silaha, lakini alikana vikali shutuma hizo.

Mamlaka ya uendeshaji mashtaka (NPA) ilidai kuingiliwa kati na wanasiasa katika uchunguzi wao na kushindwa kuendelea na kesi.

Chama kikuu cha upinzani kimekuja na hatua hii mpya ya kupinga maamuzi ya Mahakama kuu baada ya takriban miaka sita ya vita vya kisheria.

Chama tawala nchini humo kimesema Rais Zuma hayumbishwi na madai hayo waliyodai ni kichekesho