China na ukosefu wa ajira

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafanakazi wakiwa kiwandani China

China wiki hii imetangaza kuwa wafanyakazi milioni 1.8 wanaweza kuacha kazi kutokana na kudorora kwa uchumi.

Majimbo yenye kuzalisha zaidi chuma na makaa ndio yanayotarajiwa kuumia zaidi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kiasi cha wafanyakazi milioni 1.8 kwenye viwanda vya vyuma na makaa, asilimia 15 ya nguvu kazi wanatarajia kupunguzwa, kama sehemu ya juhudi za kupunguza kuelemewa kwa viwanda na pia kufuatia maafikiano ya shughuli za kiviwanda nchini humo.

Lakini kiasi cha cha watu wasio na ajira ni cha chini na hata ukosefu wa ajira nchini humo hautasababisha nchi hiyo, kuwa na kiasi kikubwa cha watu wasio na ajira, miongoni mwa mataifa yanayokabiliwa na tatizo hilo kwa kiasi kikubwa kwenye soko la ajira.

Takwimu mpya za kiuchumi kutoka China zinathibitisha kuwa uchumi wa nchi hiyo unaendelea kupungua nguvu.

Kiwangi cha wasio na ajira nchini China ni asilimia 4.7, ambacho ni cha chini katika orodha ya Shirika la kazi duniani ILO.

Katika shirika hilo la ILO nchi 120 zinaonesha kuwa na kiwango kikubwa cha watu wasio na ajira zaidi ya China.

Miongoni mwa nchi zenye tatizo kubwa la ajira ni pamoja na Afrika kusini na Mauritania, ambapo Afrika kusini ni ya tatu katika bara la Afrika.