Shell yashtakiwa Nigeria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Madhara ya umwagikaji mafuta Niger Delta

Jamii za Bille na Ogale zinasema umwagikaji huo wa mafuta umeharibu mashamba na maeneo ya kuvua samaki.

Hii ni mara ya pili katika maika mitano Shell inashtakiwa katika mahakama ya Uingereza ka umwagikaji mafuta katika eneo hilo la Niger Delta.

Jamii hizo mbili zilizowasilisha kesi zinasema maisha yao yaliharibiwa na umwagikaji huo wa mafuta na kwamba hawajapata maji safi ya kunywa kwa zaidi ya miaka ishirini na tano

Kesi iliyosikizwa London Jumatano itabaini iwapo kesi hiyo dhidi ya tawi la kampuni hiyo Nigeria inaweza kuendelea kuhudumu.

Image caption Ni mara ya pili Shell inashtakiwa kwa uchafuzi mazingira

Katika taarifa yake, Shell imesema nimapema mno kukagua madai hayo.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanaishutumu Shell kushindwa kusafisha uchafu katika Niger Delta ulio na athari kubwa kwa jamii zilizopo kwenye eneo hilo.

Image caption Makaazi ya Shell huko Niger Delta

Shell inasema uchafuzi mkubwa unatokana na wizi wa mafuta unaotekelezwa.

Lakini mwaka 2015 kampuni hiyo ilikubali kutoa dola milioni nane kama fidia kwa walioathirika na umwagikaji mafuta mkubwa uliotokea 2008.