Mamia wautoroka mji wa Dusamareb Somalia

Image caption Vita nchini Somalia

Mamia ya raia wanautoroka mji uliopo katikati ya Somalia wa Dusamareb baada ya mapigano makali kuzuka kati ya makundi hasimu ya wapiganaji,kulingana na mwandishi wa BBC Ibrahim Aden mjini Mogadishu.

Makundi hayo mawili yamedaiwa kutumia silaha kali katika maeneo ya watu wengi huku yakipigania udhibiti wa mji huo.

Hakuna ripoti za majeraha kufikia sasa.