Waasi wa LRA, waendelea kuteka watoto

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Joseph Kony

Kundi la waasi la LRA limewateka nyara watu 217 katika Jamhuri ya Afrika ya kati, toka kuanza kwa mwaka huu.

Shirika la Invisible Chldren limesema kati ya hao, watoto ni 54 ambao wanatumika kama askari, wafanyakazi ndani ya kambi zao na wale wanaotumiwa kingono.

Utekaji nyara huo unaelezwa pia ni kama jaribio la kutaka kujazia jeshi lake.

Kundi hilo limekuwa likihangaika kujipanga upya, tangu majeshi ya kigeni yalipoanza mashabulizi dhidi yake mwaka 2011.

Marekani ilipeleka kikosi maalumu cha wanajeshi 100 mwaka 2011, kuunga mkono maelfu ya wanajeshi wa Afrika wanaowasaka makamanda wake, akiwemo kiongozi wao Joseph Kony.