Soko la Filamu Tanzania litaimarika?

Image caption Tango Tv imeingia kwenye soko la kusambaza filamu Tanzania

Japo kuwa miongoni mwa tasnia kubwa Zaidi Afrika mashariki na Kati tasnia ni filamu Tanzania pamoja na watengeza filamu wanakutana na matatizo ya usambazaji usio lipa na uharamia. Lakini kampuni chipukizi ya Tango Tv imeingia kwenye soko na kuanzisha huduma ya kusambaza filamu kwa njia ya mtandao wa intanet.

Je huduma hii ni suluhisho kamili?

Wajasiriamali Victor Mnywami na Moses Kabungo wanasema king'amuzi cha Tango TV kinafunugua milango katika shughuli za usambazaji wa filamu kwa mafanikio.

Wakiwa na Zaidi ya filamu mia 200 kwenye maktaba yao, wajasiriamali hawa wamelenga pia utazamaji kwa njia ya simu na kuzindua huduma yao katika simu za mkononi , wakati wakitafuta wawekezaji wakutengeneza ving'amuzi Zaidi.

Seko Shemto ni mtarayishaji wa filamu wa kujitegemea, akiwa na uzoefu wa Zaidi ya miaka mitano katika tasnia ya filamu Tanzania, anasema uwepo wa huduma kama ya Tango ni jambo zuri kwa watazamaji lakini huduma hiyo inazua maswali na migongano kuhusu makubaliano kati ya wasambazaji na wadau wa filamu na maslahi yake.

Ukuaji wa mtandao wa intanet nchini Tanzania ni mkubwa, hadi kuwavutia wawekezaji wakubwa kama vile Netflix kutangaza kuanzisha huduma yao ya kusambaza filamu kwa njia ya mtandao barani Afrika hivi karibuni. Edwin Bruno ni mtaalam wa masuala ya teknolojia anasema uwekezaji wa makampuni makubwa kama Netflix hauwezi tishia kampuni chipukizi kwa sababu wao ndo wanafahamu Zaidi mahitaji wa wateja.