Aliyekuwa rais wa Brazil akamatwa

Image caption Lula da Silva

Maafisa wa polisi nchini Brazil wamemkamata aliyekuwa rais wa taifa hilo Luiz Inacio Lula da Silva ikiwa ni mpango wa kuchunguza ufisadi.

Mali zote zinazohusishwa naye ikiwemo nyumba yake na taasisi ya Lula zimevamiwa.

Uchunguzi huo unalenga kampuni ya mafuta ya serikali ,Petrobas.

Lula atahojiwa kuhusu madai kwamba alifaidika na mpango wa hongo uliokuwa ukiendeshwa na kampuni hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption rais wa Brazil Dilma Rouseff na Lula da Silva

Mda mchache kabla ya uvamizi huo Taaisi ya Lula ilisema kuwa rais huyo wa zamani alikana makosa yote.

Lula da Silva alihudumu kama rais kutoka mwaka 2003 hadi 2011.Mrithi wake Dilma Rousseff alihudumu kama mkuu wake wa wafanyikazi.