Kinga ya mwili kutibu saratani?

Haki miliki ya picha
Image caption Saratani ya mapafu

Wanasayansi wanaamini wamegundua njia ya kuimarisha kinga ya mwili kuangamiza saratani.

Watafiti katika chuo kikuu cha London wamepata njia ya kutafuta alama katika uvimbe,na kuiruhusu kinga ya mwili kuulenga ugojwa huo.

Lakini mbinu hiyo ya kibinafsi ilioripotiwa katika jarida la sayansi ni ghali mno na haijajaribiwa miongoni mwa wagonjwa.

Wataalam wamesema kuwa mpango huo ni mzuri lakini huenda ni mgumu kutekeleza.

Lakini watafiti ambao kazi yao imefadhiliwa na kituo cha utafiti nchini Uingereza ,wanaamini ugunduzi wao huenda ukawa uti wa mgongo wa tiba mpya na inataraji kuijaribu mbinu hiyo katika wagonjwa katika kipindi cha miaka miwili.

Wanaamini kwa kuchunguza chembe chembe za vinasaba vya DNA,wataweza kubuni tiba.