Dola bilioni 20 za Nigeria zafichwa ugenini

Haki miliki ya picha cbn facebook page
Image caption Benki kuu ya Nigeria

Benki kuu ya Nigeria imesema kuwa baadhi ya matajiri nchini humo wameficha dola bilioni 20 katika akunti zao za kubadilishana fedha za kigeni.

Gavana wa Benki Godwin Emefiele amewaambia mawakili kwamba ufichaji huo unatishia thamani ya sarufu ya Nigirea,Naira.

Onyo hilo linajiri huku serikali na benki kuu zikijaribu kudumisha thamani ya sarufi hiyo ambayo kwa sasa inabadilishana Naira 200 kwa dola moja.

Bwana Emefiele pia amedai kwamba watu fulani wanaharibu thamani ya Nair kupitia uvumi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Fedha za Nigeria

Nigeria hutegemea sana mauzo ya mafuta ili serikali kupata mapato pamoja na fedha za kigeni.

Kushuka kwa bei ya mafuta kumepunguza hifadhi ya fedha za kigeni za taifa hilo.