Dj ahukumiwa miaka 20 kwa mauaji ya mpenziwe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Klabuni

Aliyekuwa DJ wa redio ya Jozi FM Donald Sebolai amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Alipatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Dolly Tshabalala.

Akiwa amevalia shati la rangi ya buluu, Sebolai alilia.Alikumbatiwa na familia yake iliokuwa katika mahakama hiyo.

Jaji huyo alisema kuwa anaamini kwamba hukumu kali ilihitajika.