Uchina yaweka malengo ya ukuaji wa uchumi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mkutano wa Uchina

Uchina inasema kuwa inatarajia uchumi wa taifa lake kukua kati ya asilimia sita u nusu na saba mwaka huu.

Utakuwa umeongezeka ikilinganishwa na asilimia sita mwaka uliopita,kiasi cha chini sana kwa muda wa robo karne iliyopita.

Akifungua rasmi Baraza Kuu la Chama cha National People's Congress, Waziri Mkuu Li Kiegang, alianza mipango aliyosema inatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi.

Miongoni mwa hatua hizo ni kujenga barabara njema na reli na kuwapunguzia wawekezaji kodi kibinafsi na katika viwanda wanavyoekeza nchini.

Yeye pia alizungumzia juu ya haja ya kukarabati miradi ya Serikali.