Polisi wavamia gazeti kubwa Uturuki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Gazeti Uturuki

Polisi nchini Uturuki wametumia moshi wa kutoa machozi kupita miongoni mwa waandamanaji kuingia katika makao makuu ya gazeti kubwa zaidi nchini humo la Zaman baada ya Serikali kunyakua usimamizi wake.

Idara ya mashauri ya kigeni ya Marekani imesema kuwa hiyo ni mojawapo ya hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Uturuki kujaribu kusimamia idara ya mahakama na taasisi za habari nchini humo.

Mhariri mkuu wa Gazeti hilo, AbdulHamin Bilici alisema huo ni wakati wa kusikitisha kwa taifa hilo na demokrasia kwa ujumla.

Udhibiti wa gazeti hilo, vyombo vya habari vinasema, ni hatua ya kukabiliana na wafuasi wa mhubiri Mwislamu anayeishi Marekani, Fetullah Gulen.