Vikosi vya kukabiliana na itikadi kubuniwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi wa Afrika

Vikosi maalum vitabuniwa magharibi mwa Afrika katika jimbo la Sahel ili kukabiliana na tishio la itikadi kali.

Mawaziri wa ulinzi kutoka Mali,Chad,Niger,Burkina Faso na Mauritania walisema kuwa watashirikiana ili kuanzisha vikosi hivyo vitakavyoshrikisha wanajeshi 100 waliopata mafunzo makali.

Vikosi hivyo vitakavyofadhiliwa na muungano wa Ulaya EU vitafanya kazi kama vikosi vya Uhispania vilivyobuniwa ili kukabiliana na wapiganaji wa Wanaotaka kujitenga wa Basque.

Makundi yanayohuishwa na kundi la Al Qaeda yamevamia hoteli nchini Mali na Burkina Faso.

Kund la wapiganaji la Boko Haramkila mara hushambulia majirani wa taifa hilo kaskazini mashariki.