Wakataa mali ya thamani kupewa kanisa Italia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wakataa mali ya thamani kupewa kanisa Italia

Maandamano yamefanyika nje ya kanisa la Naples huko Italia kupinga agizo lililotolewa litakaloiwezesha kanisa katoliki nchini humo kupewa udhibiti wa shehena ya vyombo na vitu vya thamani ambavyo vimekuwa mikononi mwa baraza la mji kwa miaka mingi.

Image caption Maandamano yamefanyika nje ya kanisa la Naples huko Italia

Maelfu ya waandamanaji hao wamekuwa wakipeperusha vitambaa vyeupe wakisema .

''Usithubutu San Gennaro''--San Gennaro ndio jina la kiongozi wa kidini katika eneo hilo ambae alituzwa shehena hiyo yenye thamani kubwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Badhi yavyo ni vitambaa vya kichwa vya kidini vilivyonakshiwa almasi, ruby ,lozy

Miongoni mwavyo ni mikufu ya almasi, vitambaa vya kichwa vya kidini vilivyonakshiwa almasi, ruby ,lozy na vitu vyenginevyo vya thamani.

Waziri wa mambo ya nje wa Italia Angelino Alfano, amesisitiza shehena hiyo itaorodheshwa kama bidhaa za kidini wala sio mapambo ya sanaa.