Mkewe Ronald Regan,Nancy,ameaga dunia 94

Haki miliki ya picha Eric Thayer Getty
Image caption Mkewe Ronald Regan,Nancy,ameaga dunia 94

Mke wa rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan,Nancy amefariki akiwa na umri wa miaka 94.

Aliwahi kuwa mchezaji sinema, kabla ya kukutana na mumewe, Ronald , ambaye alikuwa rais wa Marekani baina ya mwaka wa 1981 na1989.

Kuna watu wanaosema, alikuwa na kauli kubwa kwa rais Reagan alipokuwa katika uongozi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ronald Regan,na mkewe Nancy

Nancy Reagan alikuwa mrembo aliyefuata mitindo ya mavazi - alianzisha kampeni ya kupambana ma mihadarati - iliyokuwa na nembo " Sema sitaki tu".