China yaonya Taiwan dhidi ya uhuru

Haki miliki ya picha AP
Image caption China yaonya Taiwan dhidi ya uhuru

Rais wa Uchina Xi Jinping ameonya kuwa kamwe hatairuhusu 'Jimbo la Taiwan' kuwa taifa huru.

Matamshi ya bwana Xi yamekuja miezi miwili baada ya kisiwa hicho kumchagua raisi mpya Tsai Ingwen.

Rais huyo mteule ataapishwa mwezi Mei mwaka huu.

Taiwan ilijitenga toka China mwaka wa 1949 baada ya kumalizika kwa vita vya wenyeye kwa wenyewe.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais huyo mteule ataapishwa mwezi Mei mwaka huu.

Tangu hapo Taiwan inajitawala yenyewe lakini mataifa mengi hayajatambua utaifa wao.

Uchina imeionya Taiwan kwamba itatumia nguvu endapo itaendelea na harakati hizo za kujitangazia kuwa taifa huru.