Trump na Cruz watoshana nguvu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Trump na Cruz watoshana nguvu

Wagombea wakuu,katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa Marekani,kwenye chama cha Republican wameshinda majimbo mawili kila mmoja katika kura ya mchujo ya hivi karibuni.

SenetaTed Cruz ameshinda majimbo ya Kansas na Maine huku bwenyenye Donald Trump, akitwaa majimbo ya Louisiana na Kentucky.

Trump tayari ameshashinda majimbo mengine kadhaa ya awali na anaongoza wapinzani wake katika Republican, jambo linalowatia wasiwasi mkubwa vigogo wa chama hicho ambao wamefadhaisha na sera tata na za uchokozi anazoziendeleza Trump, wengi wakisema zinakwenda kinyume na maadili ya Marekani.

Sasa Cruz anasema yeye ndiye anaweza kuwa mgombea mbadala wa billionaire huyo wa New York Trump.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Trump na Cruz wanawataka wagombea wenza wajiondoe iliwakabiliane moja kwa moja

Kwa upande wa chama cha Democratic bi Hillary Clinton ameshinda Louisiana,huku mpinzani wake senator Bernie Sanders akishinda Kansas na Nebraska.

Akihutubia wapinzani wake amesema demokrasia ya Marekani haipaswi kuharibiwa na mabillionare.