Yanga na Azam hakuna Mbabe

Image caption Yanga 2-2 Azam

Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara imendelea tena jana kwa michezo sita, katika uwanja wa taifa Dar es salaam mechi kati ya Yanga na Azam ilimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu mabao 2-2.

Kwa upande wa Yanga magoli yao yalifungwa na wachezaji Juma Abdul na Dolnad Ngoma.

Kwa upande wa Azam,magoli yalifungwa na John Boko na Juma Abdul likiwa ni goli la kujifunga .

Kufuatia matokeo hayo mpaka sasa Yanga inaongoza ligi kwa uwingi wa magoli huku timu zote zikiwa na pointi sawa (47).

Matokeo ya michezo mingine

African Sports imetoka sare ya bila kufungana na Maji Maji (0-0) ,Toto Africans imetoka sare na Ndanda fc (0-0), Kagera Sugar sare na Mambo Jkt (1-1),

Tanzania prison imeibamiza Stand United bao (1-0),Mtibwa imeikung'uta Coastal United mabao (3-0).

Ligi hiyo inaendelea tena Leo jumapili Machi 06 kwa mchezo mmoja Simba itaivaa Mbeya City katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.