Bomu la laptop lalipuka Somalia

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Bomu ya Laptop yalipuka Somalia

Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.

2 kati ya wale waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia.

Bomu hilo linaaminika kuwa lilikuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).

Mtu aliyekuwa ameibeba bomu hilo alikuwa anajaribu kuingia katika eneo salama katika eneo la upekuzi la Beledweyne takriban kilomita 325km nje ya Mogadishu.

Haki miliki ya picha Darren Howe
Image caption Mwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al- Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria.

Mwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al-Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria.

Shambulizi hilo lilitekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).

''Afisa wa ulinzi katika eneo hilo Luteni Kanali Ali Dhuh Abdi amesema kuwa bomu hilo lililipuka kisha maafisa wa usalama wakaharibu mabomu mengine 2 yaliyokuwa yametegwa ndani ya kipiga chapa (printer)