Zuma taabani kwa matamshi dhidi ya wanawake

Haki miliki ya picha
Image caption Zuma taabani kwa matamshi dhidi ya wanawake

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameshtumiwa kwa kutoa matamshi yanayowabagua wanawake kijinsia.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini kinadai kuwa Zuma aliwadhalilisha waandishi wanawake juma lililopita aliposema kuwa ni vigumu kwa wanaume siku hizi kuwatambua wanawake warembo.

Nikisema kuwa wewe ni mrembo katika ulimwengu huu wa wazungu unajitia katika hatari ya kushtakiwa kwa kumdhalilisha mwanamke ''

Itakuwaje ?

''Zamani ningekueleza 'Gqezu, Gqezu ntomazane! Nongenazo izinkomo uyayidla inyama',"

Tafsiri ya Zulu kuwa ,''Japo sina mali ya kutosha ya kugharamia malipo ya mahari, naomba nikuoe'' jarida la News24 linamnukuu rais huyo.

''Kama mngeturuhusu tuwatambue,bila shaka hata hawa walinzi wangu wangewaeleza jinsi mlivyo warembo.''

Haki miliki ya picha
Image caption Msemaji wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) Phumzile Van Damme alituhumu Zuma kwa matamshi hayo

''Lakini sikuhizi thubutu, utashtakiwa hapa kwa kumdhulumu mwanamke wa wenyewe kijinsia''

''Mtawakosa wanaume wazuri sana wenye nia ya kuwaoa eti kwa sababu ya haki zenu za msingi'' alisema Zuma akicheka.

Yamkini Zuma,mwenye wake 4 alitoa matamshi hayo akiambatana na mkewe, Tobeka Madiba Zuma,na mwanaye mwenye umri wa miaka 8 katika hafla hiyo ya kuwahamasisha wapiga kura kujiandikisha katika maeneo ya KwaZulu-Natal.

Msemaji wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) Phumzile Van Damme alituhumu Zuma kwa matamshi hayo.