Vazi la michezo lenye hijab nchini Afghanistan

Haki miliki ya picha hummel.net
Image caption Vazi la hijab katika michezo

Kampuni ya Hummel imetangaza ushirikiano mpya na shirikisho la soka nchini Afghanistan katika mpango ambao pia utasaidia kikosi cha taifa cha timu ya soka ya wanawake waliovalia hijab ambazo hutengezwa na kuwa katika vazi la michezo.

Kampuni hiyo ya jezi za michezo ya Denmark ilichaguwa siku ya kimataifa ya wanawake kuzindua vazi hilo jipya la wanawake litakaloorodhesha hijab ikiwa ni juhudi ya kuwavutia wanawake wengi ili kuweza kushindana na wanawake wenzao kimataifa.

Ubunifu huo unashirikisha turathi za Afghanistan na utamaduni huku hijab ikiwa kinguo kitakachowaruhusu wanawake kufunikwa kutoka kichwani hadi miguuni bila ya kuathiri uwezo wao wa kucheza.

Hatua hiyo ni ya kwanza kwa jezi ya michezo kushirikisha hijab.

Mmiliki wa Hummel Christian Stadil amesema kuwa chapa hiyo inaamini kwamba iwapo unataka kufanya mabadiliko muhimu,ni sharti ukutane na mataifa pamoja na utamaduni ulipo.