Msichana auguza majeraha ya ubakaji India

Image caption Ubakaji India

Maafisa wa polisi nchini India wamemkamata mtu mmoja baada ya msichana mmoja kudaiwa kubakwa na baadaye kuchomwa nyumbani kwake huko Greater Noida,karibu na mji mkuu wa Delhi.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 kwa sasa anapigania maisha yake hospitalini akiwa na vidonda vya moto asilimia 80.

Mshukiwa,Ajay Sharma alimtaka msichana huyo kukutana naye katika ngazi za nyumba yake ambapo anadaiwa kum'baka na kumchoma,kulingana na afisa mkuu wa polisi Rakesh Yadav ambaye aliambia BBC Hindi.

''Mshukiwa alijulikana na mwathiriwa,''bwana Yadav alisema.Aliongeza kwamba kesi ya ubakaji na jaribio la mauaji ilisajiliwa dhidi ya Ajay Sharma.

Usalama umeimarishwa katika kijiji cha Tigri ambapo kisa hicho kilitokea.

Bwana Yadav amesema kuwa anashuku kwamba kuna mchezo wa mapenzi unaondelea,na kuongezea kwamba uchunguzi zaidi unaendelea.