Netanyahu akana kuvunja mkutano na Obama

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Netanyahu na Obama

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepinga madai ya ikulu ya rais nchini Marekani kwamba ilishangazwa na hatua ya kulikataa ombi la mazungumzo na rais Barrack Obama wa Marekani.

Maafisa wa Marekani walilalamika siku ya jumatatu kwamba walibaini kupitia vyombo vya habari kuwa Benjamin Natenyahu alivunja safari yake ya kuelekea Washington wiki ijayo.

Lakini afisi ya bwana Netanyahu imesema kuwa balozi huyo wa Israel alikuwa amesema siku ya ijumaa kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba atakatiza ziara hiyo.

Uhusiano kati ya Netanyahu na Obama umekuwa wa mvutano.

Mwaka uliopita ,ikulu ya Whitehouse ilimshtumu kiongozi huyo wa Israel kwa kukiuka itifaki za kidiplomasia kupanga kulihutubia bunge la Marekani bila kumjulisha rais Obama.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Netanyahu

Alitumia hotuba hiyo ili kuwataka wabunge wa Marekani kukataa makubaliano ya kinyuklia na Iran.

Bwana Netanyahu alitarajiwa kuzuru Washington ili kuhutubia mkutano wa kila mwaka wa kamati ya maswala ya uma kati ya Israel na Marekani.

Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa waziri mkuu Netanyahu alikuwa amependekeza siku mbili za mazungumzo na Obama na kwamba mojawapo iliingiliana na mpango wa rais Obama.