Nike yasimamisha uhusiano na Sharapova

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sharapova

Kampuni ya Nike imesimamisha kwa mda uhusiano wake na bingwa mara tano wa tenisi Maria Sharapova baada ya mchezaji huyo kukiri kupatikana na dawa za kusisimua misuli.

Kampuni hiyo imesema kuwa imeshangazwa na kukiri kwake kwamba alipatikana na dawa hizo katika michuano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.

''Tumeamua kusitisha uhusiano wetu kwa mda huku uchunguzi ukiendelea ,ilisema.Tutandelea kuangalia hali ilivyo''.

Uhusiano wa Sharapova na Nike ulianza akiwa miaka 11.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sharapova

Mwaka 2010,mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Urusi aliweka kandarasi ya miaka minane na kampuni hiyo ya jezi za michezo iliokuwa na thamani ya dola milioni 70 pamoja na malipo ya nguo zake za kibinafsi.

Bi Sharapova ndiye mchezaji wa kike anayelipwa fedha nyingi baada ya kupokea dola milion 30 mwaka 2015 kutokana na ushindi pamoja na ufadhili kulingana na Forbes.

Hii inashirikisha kandarasi na Evian ,Tag Heur,Porshe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sharapova

Mwaka 2014,Porsche ilimtaja kuwa mwanamke wa kwanza kuwa balozi wake .Bi Sharapova ambaye anaishi mjini Florida pia ni sura ya manukato ya Avon na Luck.