Ofisi za kandanda zavamiwa Paris

Image caption Uswisi inamchunguza Blatter

Ofisi ya mkuu wa sheria nchini Uswisi imethibitisha kuwa utawala nchini Ufaransa umevamia ofisi za shirikisho la kandanda mjini paris.

Uvamizi huo wa siku ya Jumanne una uhusiano na uchunguzi unaoendeshwa na uswisi kwa mkuu wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Sepp Blatter.

Maafisa hao walichukua stakabadhi zinazohusiana na malipo ya dola milioni mbili yaliyofanywa na bwana Blatter kwa mkuu wa shirikisho la kandanda barani ulaya Michel Platini.