Waandamana kupinga ubakaji Nigeria

Image caption Takriban visa 30 vya ubakaji huripotiwa kila wiki katika jimbo hilo

Wanawake wameandamana katika mitaaya mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria kupinga visa vya ubakaji vinavyoongezeka.

Waandamanaji hao wakiwemo wanawake mawakili na viongozi wa kidini, waliutaka utawala kufanya jitihada zaidi ili kuwalinda watoto wadogo na kuhakikisha kuwa wahusika wamefikishwa mbele ya sheria.

Takriban visa 30 vya ubakaji huripotiwa kila wiki katika jimbo hilo.

Mama mmoja wa mtoto wa umri wa miaka 13 anasema kuwa mwanawe bado amethirika kisaikolojia tangu abakwe na mwanamme wa umri wa miaka 35 mwezi Januari mwaka uliopita.