Korea yadai kuunda bomu la kinuklia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kim Jong-un

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amedai kuwa wanasayansi wake wamefanikiwa kubuni zana za kinuklia tayari kutundikwa kwenye mizinga ya masafa marefu.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali limechapisha picha zinazomuonyesha bwana Kim akisimama karibu na kifaa chenye umbo la mstatili.

Mwandishi wa BBC aliyepo katika eneo hilo amesema ni vigumu kuthibitisha madai hayo kama ni ya kweli.