Slovenia yaidhinisha sheria mpakani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sheria hizo ni za kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Human Rights Watch limeshutumu mataifa ya Ulaya kwa kufunga mipaka yake kwa wahamiaji wakati ambapo Slovenia imedihinisha sheria mpya za mpakani kwa wahamiaji.

Ni wahamaiji wanaotafuta hifadhi pekee nchini humo au wanaowasili mpakani kutafuta usaidizi wa kibinadamu ndio watakaoruhusiwa kuingia.

Njia kuu kutoka Ugiriki hadi Ulaya kaskazini inafungwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Nyaya zimewekwa katika mpaka wa Slovenia

Takriban watu laki tano wamepitia Slovenia ambayo ni nchi mwanachama Wa Umoja wa Ulaya tangu msimu wa mapukutiko.

Lakini sasa serikali ya Slovenia inashika breki. Inasema itaidhinisha sheria hizo ya mipaka wazi Ulaya na itawaruhusu watu wanaoomba hifadhi pekee nchini humo.

Wazir mkuu wa Slovenia Miro Cerar amesema hatua hiyo itasababisha kufungwa kikamilifu kwa njia ya Balkan kwa wahamiaji.

Serbia, nchi nyengine iliopo kwenye njia hiyo ya Balkan imesema itaoanisha sera zake na Slovenia na kuidhinisha sheria kama hizo.