Waziri wa ujenzi akemea kuchati TZ

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mitandao ya whatsapp na Facebook

Waziri wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi nchini Tanzania Makame Mbarawa amekemea tabia za wafanyakazi wa umma kutumia muda wao mwingi wa kazi kuchat mitandaoni.

"Hapa kuna wateja wamefika wanataka huduma wewe una chati sio sahihi'' alisema bwana Mbarawa.

''Tumepewa kazi hizo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi" Aliendelea kusema Mbarawa.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya.

Aidha amewataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.

Image caption Watu wengi hutumia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali na pia kujifunza.

Lakini hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?

Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza na kujiburudisha.

Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogu mbalimbali.