Trump ashinda Mississipi na Michigan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Mgombea anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi.

Wadadisi wanasema kuwa ushindi huo mara mbili umezima uvumi wa mwishoni mwa wiki kuwa kampeni yake Trump ilikuwa imepoteza kasi.

Baada ya kupata ushindi huo , Trump alisema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican. Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye alipata ushindi katika jimbo dogo la Idaho.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bernie Sanders na Hillary Clinton

Kwenye upande wa chama cha Democratic inaripotiwa kuwa Bernie Sanders ameshinda mchujo katika jimbo la Michigan huku naye Hillary Clinton akiibuka mshindi katika jimbo la Mississipi.