Apple yashinikizwa kuifungua simu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Apple

Utawala nchini Marekani unakata rufaa kupinga uamuzi wa jaji wa kukosa kuamrisha kampuni ya Apple kuifungua simu ya mkononi katika kesi moja inayohusu madawa ya kelevya.

Wizara ya sheria inatumia sheria sawa na iliyotumia katika majaribio yake ya kwanza ya kuitaka Apple kuifungua simu ya mwanamgambo aliyetekeleza mauaji katika eneo la San Bernardino.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Simu za Apple

Serikali ilienda mahakamani baada ya jaji katika neo la Brooklyn kusema kuwa hakuwa na mamlaka ya kutoa amri kama hiyo.

Katika kesi hiyo, serikali ya Marekani inamtaka jaji kuamrisha Apple iifungue simu ya Jun Feng, ambaye alikiri kuhusika katika ulangusi wa madawa ya kulevya.

Inataka kutumia simu hiyo kuwanasa baadhi ya washirika wake.