Mtaalam wa kemikali wa IS akamatwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Mtaalamu wa maswala ya silaha za kemikali katika wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq amekamatwa na vikosi maalum vya Marekani na sasa anahojiwa.

Mtu huyo alikuwa mtaalamu wa maswala ya silaha za kibaiolojia wa aliyekuwa rais wa Iraq Sadam Hussein ,aliyependuliwa na uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003,duru za Iraq na zile za Marekani zimeambia vyombo vya habari vya Marekani.

Akijulikana kama Sleiman Daoud al_fari,aliripotiwa kukamatwa mwezi uliopita.

Hatahivyo,msemaji wake amesema kuwa vikosi maalum vya Marekani vimeanza oparesheni zake nchini Iraq,ikiwa ni mwanzo wa vita vikali dhidi ya Islamic State.

Mtu huyo amewaambia wanaomuhoji vile kundi la Islamic State lilivyotumia gesi ya sumu katika makombora yake,duru za Marekani zimeambia gazti la The New York Times.